Diamond Platnumz kuwania tuzo ya BET

0
1154

Nyota wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul, maarufu Diamond Platnumz ametajwa katika orodha ya wasanii wanaowania tuzo za BET nchini Marekani kwa mwaka 2021.

Diamond ametajwa katika kipengele cha Mwanamuziki Bora wa Kimataifa (Best International Act) akiwa pamoja na wasanii wengine ambao ni Wizkid na Burna Boy wote kutoka Nigeria.

Wengine katika orodha hiyo ni Aya Nakamura wa Ufaransa, Emicida wa Brazil, Headie One wa Uingereza, Young T & Bugsey wa Ungereza na Youssoupha wa Ufaransa.

Hii ni mara ya tatu kwa Diamond Platnumz kuwania tuzo hiyo, ambapo alitajwa katika orodha ya mwaka 2014 na 2016 (kwa upande wa Afrika). Mwaka 2014 mwanamuziki Davido aliibuka mshindi, huku Black Coffee akishinda tuzo hiyo mwaka 2016.

Tuzo hiyo sasa inashikiliwa na Burna Boy ambaye ndiye aliitwaa mwaka 2020.

Tuzo za BET zitafanyika Juni 27 na watu watahudhuria tamasha hilo baada ya mwaka jana kufanyika kwa njia ya video kutokana na mipuko wa virusi vya corona.

Hapa chini ni orodha kamili ya wasanii wanaowania tuzo hizo pamoja na vipengele husika;

ALBAMU BORA YA MWAKA

AFTER HOURS – THE WEEKND
BLAME IT ON BABY – DABABY
GOOD NEWS – MEGAN THEE STALLION
HEAUX TALES – JAZMINE SULLIVAN
KING’S DISEASE – NAS
UNGODLY HOUR – CHLOE X HALLE

USHIRIKIANO BORA (BEST COLLABORATION)

CARDI B FT. MEGAN THEE STALLION – WAP
DABABY FT. RODDY RICCH – ROCKSTAR
DJ KHALED FT. DRAKE – POPSTAR
JACK HARLOW FT. DABABY, TORY LANEZ & LIL WAYNE – WHATS POPPIN (REMIX)
MEGAN THEE STALLION FT. DABABY – CRY BABY
POP SMOKE FT. LIL BABY & DABABY – FOR THE NIGHT

MSANII BORA WA KIKE WA R&B / POP

BEYONCÉ
H.E.R.
JAZMINE SULLIVAN
JHENÉ AIKO
SUMMER WALKER
SZA

MSANII BORA WA KIUME WA R&B / POP

6LACK
ANDERSON .PAAK
CHRIS BROWN
GIVEON
TANK
THE WEEKND

MSANII BORA CHIPUKIZI

COI LERAY
FLO MILLI
GIVEON
JACK HARLOW
LATTO
POOH SHIESTY

KUNDI BORA

21 SAVAGE & METRO BOOMIN
CHLOE X HALLE
CHRIS BROWN & YOUNG THUG
CITY GIRLS
MIGOS
SILK SONIC

MSANII BORA WA KIKE WA HIP HOP

CARDI B
COI LERAY
DOJA CAT
MEGAN THEE STALLION
LATTO
SAWEETIE

MSANII BORA WA KIUME WA HIP HOP

DABABY
DRAKE
COLE
JACK HARLOW
LIL BABY
POP SMOKE

‘BOBBY JONES BEST GOSPEL/INSPIRATIONAL AWARD’

BEBE WINANS – IN JESUS NAME
CECE WINANS – NEVER LOST
H.E.R. – HOLD US TOGETHER
KIRK FRANKLIN – STRONG GOD
MARVIN SAPP – THANK YOU FOR IT ALL
TAMELA MANN – TOUCH FROM YOU

‘BET HER AWARD’

ALICIA KEYS FT. KHALID – SO DONE
BRANDY FT. CHANCE THE RAPPER – BABY MAMA
BRI STEVES – ANTI QUEEN
CHLOE X HALLE – BABY GIRL
CIARA FT. ESTER DEAN – ROOTED
SZA – GOOD DAYS

MSANII BORA WA KIMATAIFA

AYA NAKAMURA (FRANCE)
BURNA BOY (NIGERIA)
DIAMOND PLATNUMZ (TANZANIA)
EMICIDA (BRAZIL)
HEADIE ONE (UK)
WIZKID (NIGERIA)
YOUNG T & BUGSEY (UK)
YOUSSOUPHA (FRANCE)

‘VIEWER’S CHOICE AWARD’

CARDI B FT. MEGAN THEE STALLION – WAP
CHRIS BROWN & YOUNG THUG – GO CRAZY
DABABY FT. RODDY RICCH – ROCKSTAR
DJ KHALED FT. DRAKE – POPSTAR
DRAKE FT. LIL DURK – LAUGH NOW CRY LATER
LIL BABY – THE BIGGER PICTURE
MEGAN THEE STALLION FT. BEYONCÉ – SAVAGE (REMIX)
SILK SONIC – LEAVE THE DOOR OPEN

VIDEO BORA YA MWAKA

CARDI B – UP
CARDI B FT. MEGAN THEE STALLION – WAP
CHLOE X HALLE – DO IT
CHRIS BROWN & YOUNG THUG – GO CRAZY
DRAKE FT. LIL DURK – LAUGH NOW CRY LATER
SILK SONIC – LEAVE THE DOOR OPEN

MWONGOZA VIDEO WA MWAKA

BENNY BOOM
BRUNO MARS AND FLORENT DÉCHARD
COLE BENNETT
COLIN TILLEY
DAVE MEYERS
HYPE WILLIAMS

FILAMU BORA

COMING 2 AMERICA
JUDAS AND THE BLACK MESSIAH
MA RAINEY’S BLACK BOTTOM
ONE NIGHT IN MIAMI
SOUL
THE UNITED STATES VS. BILLIE HOLIDAY

MWIGAZAJI BORA WA KIKE

ANDRA DAY
ANGELA BASSETT
ISSA RAE
JURNEE SMOLLETT
VIOLA DAVIS
ZENDAYA

MWIGIZAJI BORA WA KIUME

ALDIS HODGE
CHADWICK BOSEMAN
DAMSON IDRIS
DANIEL KALUUYA
EDDIE MURPHY
LAKEITH STANFIELD

‘YOUNGSTARS AWARD’

ALEX R. HIBBERT
ETHAN HUTCHISON
LONNIE CHAVIS
MARSAI MARTIN
MICHAEL EPPS
STORM REID

MWANAMICHEZO BORA WA KIKE WA MWAKA

A’JA WILSON
CANDACE PARKER
CLARESSA SHIELDS
NAOMI OSAKA
SERENA WILLIAMS
SKYLAR DIGGINS-SMITH

MWANAMICHEZO BORA WA KIUME WA MWAKA

KYRIE IRVING
LEBRON JAMES
PATRICK MAHOMES
RUSSELL WESTBROOK
RUSSELL WILSON
STEPHEN CURRY