SADC yajadili hali ya usalama Msumbiji

0
186

Mkutano wenye lengo la kujadili  hali ya ulinzi na usalama nchini Msumbiji hasa katika jimbo la Gabo Delgado umefanyika chini humo, chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) ambaye ni Rais wa Botswana,- Mokgweetsi Masisi.

Akitoa taarifa ya ufunguzi wa mkutano huo Rais Mokgweetsi Masisi ameahidi kuwa SADC itahakikisha hali ya ulinzi na usalama inarejea katika jimbo hilo la Cabo Delgado na katika nchi zote Wanachama wa SADC.

Katika mkutano huo Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewakilishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi.

Miongoni mwa makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano huo ni kuhakikisha Msumbiji inamaliza na kuondoa kabisa vitendo vya kigaidi katika jimbo hilo la Kaskazini la Cabo Delgado pamoja na kuendelea kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Tayari Rais Dkt. Mwinyi amerejea Zanzibar mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo.