Kaburi lafukuliwa, mwili wanyofolewa viungo

0
221

Mkuu wa wilaya ya Gairo mkoani Morogoro, Siriel Mchembe ameagiza kutafutwa na kukamatwa kwa watu wanaotuhumiwa kunyofoa viungo vya mwili vya marehemu Rehema Michael Mei 24, mwaka huu.

Mchembe ametoa agizo hilo kwa jeshi la polisi wilayani humo, baada ya kubaini kuwa kaburi ulimozikwa mwili wa Rehema limefukuliwa na watu wasiojulikana, na kunyofolewa viungo kikiwemo kichwa, sehemu za siri, moyo na mapafu na kisha kutokomea navyo kusikojulikana.

Rehema alifariki dunia Mei 22 kwa ajali ya gari na kuzikwa katika kijiji cha Nguyami wilayani Gairo Mei 23 mkoani Morogoro.

Mchembe amefika kwenye kaburi hilo akiwa ameongozana na Kamanda wa polisi wa wilaya ya Gairo na Mganga Mkuu wa wilaya hiyo.