Rais Yoweri Museveni wa Uganda tayari amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja, kwa mwaliko wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Akiwa hapa nchini pamoja na mambo mengine, Rais Museveni akiwa na mwenyeji wake watashuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga, Tanzania.
Mikataba hiyo inatiwa saini Ikulu jijini Dar es salaam kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni za uwekezaji katika mradi huo (Host Government Agreement).