Kiwanda cha ushonaji cha Jeshi la Polisi chazinduliwa

0
233

Rais Samia Suluhu Hassan amezindua kiwanda cha ushonaji cha Jeshi la Polisi kilichopo Kurasini mkoani Dar es salaam, ambacho kitakuwa kikishona sare za askari wa jeshi hilo.

Kiwanda hicho ambacho ni cha kisasa kitakuwa na uwezo wa kushona sare mia nane kwa siku kutoka sare mia mbili za askari polisi zilizokuwa zikishonwa hapo awali.

Zaidi ya shilingi milioni mia sita zimetumika katika ujenzi wa kiwanda hicho, ujenzi ulioanza mwezi June mwaka 2020.