Mashambulio yaendelea Gaza, vifo vyaongezeka

0
174

Israel imeendelea kufanya mashambulio kwenye Ukanda wa Gaza,  na kusababisha vifo pamoja na uharibifu wa mali mbalimbali.

Mashambulio hayo yanayofanywa na ndege za Israel, yamesababisha vifo vya takribani raia mia mbili wa Kipalestina katika kipindi cha wiki moja.

Wakati ndege za Israel zikiendelea kufanya mashambulio hayo, nao Wapiganaji wa Kipalestina wameendelea kuishambulia Israel kwa makombora.

Kufuatia kuendelea kwa mashambulio hayo kwenye Ukanda wa Gaza, Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanatarajiwa kukutana tena katika kikao cha dharura, lengo likiwa ni kujadili hatua za kidiplomasia zenye lengo la kusimamisha mashambulio hayo.