Spika Ndugai: Tutaendelea kutunga sheria nzuri

0
156

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kuwa bunge litaendelea kushirikiana na mhimili wa mahakama ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanapata fedha za kutekeleza majukumu yao kadiri bajeti itakavyowezesha.

Amesema hayo Ikulu, Dar es Salaam katika hafla ya uapisho wa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama ya Rufani na kuongeza kuwa Bunge litaendelea kutunga sheria zitazohakikisha kuwa nchi inaendelea kuwa salama.

Amewasihi kumtanguliza Mungu katika utendaji wao kwano dhamana waliyopewa ni kubwa sana, na watumia kuaminiwa huko kuwatumikia wananchi.