DC Sabaya asimamishwa kazi

0
605

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemsimamisha kazi Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazomkabili.

Sabaya amesimamishwa kazi kuanzia leo tarehe 13 Mei, 2021.

Wakati huo huo, Rais Samia amemteua Nsubili Akomeligwe Kajela Joshua kuwa Karani wa Baraza la Mawaziri. Joshua alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Rais Samia amemteua Ayub Makoye kuwa Naibu Karani wa Baraza la Mawaziri. Makoye alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Katika hatua nyingine, Rais amemteua Dkt. Stergomena Tax kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute). Dkt. Tax ni Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Rais Samia amemteua Dkt. Laurian Ndumbaro kuwa Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Uongozi. Dkt. Ndumbaro ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Sambamba na uteuzi huo, Rais Samia amefanya uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Uongozi ambao ni Balozi Ritta Swan, Prof. Penina Mlama, Lina Soiri, David Walker, Suzan Mlawi, Dkt. Hamis Mwinyimvua na Prof. Samwel Wangwe.

Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 13 Mei, 2021.

Katika hatua nyingine, Rais Samia amemteua Ishmael Andulile Kasekwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB). Uteuzi wa Bw. Kasekwa umeanza tarehe 10 Mei, 2021 na amechukua nafasi ya Dkt. Rosebud V. Kurwijila ambaye amemaliza muda wake.