Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amewahakikishia wajasiriamali wadogo kupata vitambulisho vilivyotolewa na Rais John Magufuli na kuwataka wakuu wa wilaya na maafisa biashara kusimamia zoezi la ugawaji huku akionya dhidi ya udanganyifu wowote.
Mtaka amesema hayo wakati akikabidhi vitambulisho vya wajasiriamali wadogo kwa wakuu wa wilaya za mkoa wa Simiyu.
Amesema kuwepo kwa vitambulisho hivyo kutajenga uthubutu na ujasiri na kuwaibua wajasiriamali wapya huku akisisitiza kwamba mkoa wa Simiyu umejipanga kuwafikia wajasiriamali wanyonge kama ilivyokusudiwa na Rais Magufuli.
Baadhi ya wajasiriamali wamemshukuru Rais Magufuli kwa vitambulisho hivyo na kusema vitawaondolea adha waliyokuwa wakiipata.