Uzinduzi wa mbio za mwenge kwa mwaka 2021

0
303

Uzinduzi wa mbio za mwenge kwa mwaka 2021 unatarajiwa kufanyika Mei 17 Mkoa wa Kusini Unguja.

Mbio za mwenge huzunguka nchi nzima ukiwa na ujumbe wa heshima, mshikamano, tumaini na amani na huhitimishwa Oktoba 14 katika kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mbio hizo huwa na kaulimbiu mbalimbali kila mwaka kulingana na vipaumbele vya serikali, na huzindua miradi ya maendeleo katika halmashauri ambazo hupita.