Ndugai atoa sharti wabunge kufukuzwa uanachama

0
314

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amevitaka vyama vya siasa vinavyotaka kufukuza wanachama wao ambao ni wabunge kufuata sheria na taratibu zote kwani lazima mchakato huo utendeke kwa haki.

Ndugai amesema hilo bungeni mjini Dodoma na kueleza kuwa anaposema kitu isichukuliwe kama ni Job Ndugai ndiye amesema, bali kiti cha Spika wa Bunge.

“Maamuzi ninayotoa hapa, ni maamuzi ambayo yatatumika nami na hata watakaofuata baada yangu… Kwa vyama vyovyote vyenye kufukuza wabunge…. wanapaswa wanapomwandikia barua spika… lazima barua hiyo iambatane na katiba yao, iambatane na muhtasari au mihtasari ya vikao vilivyohusika kuwafukuza wabunge hao,” ameeleza Spika.

Amesema kwa kufanya hivyo inarahisisha kazi yake ya kutenda haki.