Rais Samia Suluhu Hassan kuzungumza na Wazee

0
183

Rais Samia Suluhu Hassan, kesho anatarajiwa kuwa na mkutano na Wazee wa mkoa wa Dar es salaam.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, – Aboubakar Kunenge amewaambia waandishi wa habari kuwa, mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City kuanzia saa 8 mchana.

Kunenge ametoa wito kwa Wazee waliopata mwaliko wa kushiriki mkutano huo kujitokeza kwa wingi, ili wapate kusikiliza kile ambacho Rais Samia Suluhu Hassan amewaitia.

Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya Wazee 900 wa mkoa huo  wa Dar es salaam.