Zaidi ya shule 1,000 kujengwa

0
142

Serikali imesema ina mpango wa kujenga shule za sekondari zaidi ya 1,000 katika kutekeleza sera yake ya kuhakikisha kila kata inakuwa na shule ya sekondari.

Hayo yamebainishwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, David Silinde wakati akijibu maswali bungeni katika kipindi cha maswali na majibu.

Aidha, ameongeza kuwa serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya shule ambazo tayari zimeshajengwa ikiwa ni pamoja na kuondoa tatizo la madarasa nchi nzima.