Mourinho apewa dili AS Roma

0
164

Kocha mwenye makeke mengi Jose Mourinho ameula tena baada ya kutajwa kuwa kocha mpya wa timu ya AS Roma ya Italia kuanzia msimu ujao wa 2021 – 2022.

Mourinho mwenye umri wa miaka 58 atachukua nafasi ya Mreno mwenzie Paulo Fonseca ambae mapema leo Jumanne alitangaza kuachana na kazi hiyo mwishoni mwa msimu huu.

April 19 ya mwaka huu Jose Mourinho alifutwa kazi na timu ya Tottenham ya England na mwenywe alinukuliwa akisema atasubiri fursa nyingine na kweli imetokea na amesaini kanadarasi ya miaka mitatu kuinoa timu hiyo iliyoko kweye mjii mkuu wa Italia wa Roma.

Hii ni mara ya pili kwa Mourinho kufundisha soka nchini Italia ambapo mara ya mwisho aliinoa timu ya Inter Millan ambayo aliweza kuipa ubingwa wa Seria A mara mbili, ubingwa COPA Italia mara moja na ule wa Ulaya na mwenyewe amesema hamasa kubwa waliyonayo mashabiki wa AS Roma ndio imemchagiza mno kujiunga na timu hiyo na anasubiri kwa hamu kubwa kuianza kazi hiyo msimu ujao.