Watatu wafukiwa na kifusi na kufariki dunia

0
164

Watu Watatu wamefariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo ya moramu yaliyopo eneo la Kisongo mkoani Arusha.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Idd Kimanta ametembelea eneo la tukio na kuwaagiza Wataalam wa madini mkoani humo kwenda katika machimbo hayo na kutoa elimu ya njia salama ya kuchimba moramu hiyo.

Amesema amebaini njia inayotumika hivi sasa si salama kutokana
na kutokuwa na utaalamu wa kutosha.
 
Mkuu huyo wa mkoa wa Arusha amewataka Wachimbaji wa moramu katika eneo hilo kuendelea na shughuli za uchimbaji huku wakichukua tahadhari.

Eneo hilo la machimbo ya moramu la Kisongo lina wachimbaji zaidi ya mia tano.