Kidato cha sita kuanza mitihani kesho

0
172

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza kuanza kwa mitihani ya taifa ya kidato cha sita na ya ualimu inayotarajiwa kuanza kesho Mei 3, 2021.

Katibu Mtendaji wa NECTA, Dkt. Charles Msonde amesema jumla ya watahiniwa 90,025 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha sita ambapo kati ya hao watahiniwa wa shule ni 81,343 na watahiniwa wa kujitegemea ni 8,682.

Dkt. Msonde amezitaka kamati za mitihani za mikoa na halmashauri, manispaa, jiji, kuhakikisha taratibu zote za uendeshaji mitihani ya taifa zinazingatiwa ili kudhibiti mianya yote inayoweza kusababisha kutokea kwa udanganyifu na kuwaasa wasimamizi wa mitihani,wamiliki wa shule kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu wa mtihani huu maandalizi yote ya mitihan inakamilika.