Simba kuvaana na Kaizer Chiefs Robo Fainali

0
414

Klabu ya Simba itacheza na timu ya Kaizer Chiefs kutoka Afrika Kusini katika robo Fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Droo ya Robo Fainali imechezeshwa katika makao makuu ya CAF yaliyopo Cairo nchini Misri.

Mechi ya kwanza Simba watakuwa ugenini Kati ya Tarehe 14 ama 15 Mei na kurudiana Mei 21 ama 22 Dar es Salaam.