Aliyewahi kuwa Mbunge wa Singida Kaskazini na Waziri katika Serikali ya awamu ya Nne, Lazaro Nyalandu ametangaza kurejea katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) akitokea chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Nyalandu ametangaza uamuzi huo jijini Dodoma, wakati wa mkutano mkuu maalum wa CCM.
Akitangaza uamuzi huo, Nyalandu amekishukuru Chama Cha Mapinduzi kwa kumpokea.