Maandalizi ya mkutano mkuu maalum wa CCM yakamilika

0
181

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole amesema kuwa, maandalizi yote kuelekea mkutano mkuu maalum wa chama hicho utakaofanyika hapo kesho jijini Dodoma yamekamilika.
 
Polepole amesema kazi kubwa ya mkutano huo ni kumchagua Mwenyekiti mpya wa CCM Taifa, kufuatia kifo cha Dkt. John Magufuli aliyekuwa Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa chama hicho kilichotokea Machi 17 mwaka huu.
 
Mkutano mkuu maalum wa CCM unaofanyika hapo kesho unaratajiwa kuhudhuriwa na Wajumbe 1,876 na wageni waalikwa takribani elfu moja kutoka ndani na nje ya nchi.