Tshabalala abaki Msimbazi

0
357

Nahodha Msaidizi wa Simba SC, Mohamed Hussein Zimbwe Jr, maarufu Tshabalala amesaini mkataba mpya kuendelea kuitumikia klabu hiyo yenye makao yake Msimbazi jijini Dar es Salaam.

Tshabalala amesaini mkataba huo wakati kukiwa na tetesi kuwa angeondoka klabuni hapo na kujiunga na klabu nyingine, ambapo kwa sasa amezidi kuwa na kiwango bora katika Ligi Kuu Tanzania Bara na mechi za kimataifa.

Taarifa hiyo imetolewa na klabu Simba SC kupitia ukurasa wake wa Twitter, lakini hata hivyo haijaeleza nyota huyo amesaini mkataba wa muda gani.

“Contract extension [kuongeza mkataba]. Bado yupo sana Msimbazi,” ujumbe ulioandikwa na klabu hiyo kwenye mtandao wa Twitter.