MEI MOSI KITAIFA KUFANYIKA KIRUMBA MWANZA

0
151

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, 
Vijana na Wenye Ulemavu Jenista Mhagana amesema kuwa sherehe hizo zitafanya Kitaifa katika uwanja vya CCM Kirumba mkoani Mwanza.

Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zinafanyika Mei Mosi ya kila mwaka ili kuwapa nafasi Wafanyakazi wa sekta mbalimbali kujumuika pamoja na kujadilili masuala mbalimbali yanayowahusu.