TPA yatakiwa kuwawajibisha Watumishi wabadhirifu

0
133

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mwita Waitara, amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) Erick Hamis kutomvumilia mtumishi yoyote mbadhirifu wa mali ya umma.

Naibu Waziri Waitara ametoa kauli hiyo mkoani Tanga wakati wa mkutano wake na Watumishi wa idara za ujenzi na uchukuzi mkoani humo.

Amesema serikali ipo tayari kumvumilia mtumishi mwadilifu na si mbadhirifu.