Kimbunga Jobo kupungua nguvu siku ya Jumapili

0
227

Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) imewataka Wananchi kuzingatia taarifa na miongozo ya Wataalam wa hali hewa, ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza kutokana na kimbunga Jobo kinachoendelea kusogea kuelekea pwani ya Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi amesema kuwa, mwenendo wa kimbunga Jobo unaonesha kuwa kesho mchana kitakuwa  umbali wa kilomita 125 mashariki mwa kisiwa  cha Mafia mkoani Pwani.

Dkt. Kijazi amesema kuwa kimbunga hicho kitaanza kupungua nguvu tarehe 25 mwezi huu kitakapokuwa katika mwambao wa pwani ya Tanzania.

Kufuatia tishio la kimbunga Jobo, Dkt. Kijazi amewataka Wananchi wote, hasa wale wanaoishi katika maeneo ya pwani kutopuuza tahadhari zinazotolewa na Wataalam wa TMA kuhusu kimbunga hicho na kufuata miongozo yote inayotolewa na Wataalam hao.