Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Hedwiga Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania.
Dkt. Swai anashika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Wakati huo huo, Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Sophia Kaduma kuwa Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS).
Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo.