Boti ya mizigo yazama bandarini

0
143

Boti ya mizigo iliyotambuliwa kwa jina la Ruchugi 2 iliyobeba zaidi ya tani 120 za bidhaa mbalimbali, imezama katika bandari ndogo ya Kibirizi iliyopo katika manispaa ya Kigoma – Ujiji mkoani Kigoma.

Ajali hiyo imesababisha hasara kubwa kwa Wafanyabiashara waliokuwa wakisafirisha bidhaa hizo kwenda Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Ajali ya kuzama kwa boti hiyo ya mizigo iliyokuwa ikisafirisha bidhaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na vyakula na saruji, imetokea majira ya saa 11 alfajiri hii leo.

Ikiwa katika bandari hiyo ya Kibirizi, boti hiyo ilipigwa na wimbi kubwa na kugongwa kwenye chuma cha kivuko, na hivyo kuzama majini.