Rais Samia Suluhu Hassan : Tutailea ATCL

0
142

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali itaendelea kulilea Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na kulitua mzigo wa madeni, lengo likiwa ni kuhakikisha haliendelei kupata hasara.

Akilihutubia Bunge jijini Dodoma, Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali haiko tayari kuona shirika hilo lnaendelea kupata hasara wakati tayari umefanyika uwekezaji mkubwa ndani ya shirika hilo.

Amesema kuwa Serikali itahakikisha inaajiri Watumishi wenye uwezo wa kuliendesha Shirika hilo kwa ufanisi.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema ili ATCL ifanye kazi vizuri inahtaji kuwa na miundombinu imara, hivyo Serikali ya awamu ya sita itafanya kila liwezekanalo.kuboresha miundombinu ya shirika hilo, miundombinu inayoendana na teknolojia ya kisasa.