Yanga na Raja Casablanca kushirikiana

0
143

Klabu ya soka ya Yanga jana April 21, 2021 imeingia makubaliano ya ushirikiano na klabu ya Raja Club Athletic ya Casablanca nchini Morocco.

Ushirikiano huo utahusisha masuala mbalimbali ya maendeleo baina ya klabu hizo mbili zenye historia kubwa Barani Afrika.

Yanga imeingia makubaliano hayo ikiwa ni hatua ya klabu hiyo kujiimarisha zaidi katika soka la ushindani Barani Afrika.