Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa, leo amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) katika ofisi za Idara ya Habari Maelezo zilizopo jijini Dodoma.
Wakati wa mazungumzo yao wamesisitiza ushirikiano baina ya pande hizo mbili na pia kuwakumbusha Waandishi wa habari kuwa kipindi cha mpito kinachowataka kuwa na Diploma kinaishia Desemba 31 mwaka huu.
Hata hivyo Msigwa amewatoa hofu Waandishi wa habari kuwa wasichukulie hasi kanuni ya sheria hiyo kwa kuwa ina malengo chanya kwa taaluma hiyo nchini.
“Mtu anayelima Muhogo hawezi kulima tu bila kufuata kanuni bora za ukulima wa muhogo, hivyo itampasa kupata elimu ya namna bora ya kulima ili kupata ama kuongeza tija”, amesisitiza Msemaji Mkuu huyo wa Serikali.