Waliojifanya wana ulemavu wakamatwa

0
431

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia wanawake wawili wakazi wa Mji wa Himo ambao wanajifanya walemavu huku wakiomba omba mtaani hali ya kuwa sio walemavu.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Amon Kakwale amesema wanawake hao ambao mmoja alikuwa na mtoto mdogo walikuwa kwenye viti mwendo wakisukumwa na kupitishwa maeneo mbalimbali ya Mji wa Himo wakiomba wasaidiwe ili waweze kupata kipato.

Kufuatia tukio hilo Kamanda Kakwale amewataka wananchi kutumia viungo vyao kujipatia kipato halali na kuachana na tabia ya kuwahadaa wananchi kwa kujifanya wao ni walemavu ili wasaidiwe.

Amesema Jeshi la Polisi litawafikisha mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.