Idriss Deby atangazwa mshindi wa kiti cha Urais

0
217

Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Chad imemtangaza Idriss Deby kuwa mshindi wa kiti cha urais kufuatia uchaguzi uliofanyika tarehe 11 mwezi huu.

Idriss Deby ambaye anatetea kiti hicho, ametangazwa mshindi baada ya kupata asilimia 80 ya kura zote zilizopigwa.

Rais Idriss Deby amewania kiti hicho kwa kipindi cha sita na tayari ameliongoza Taifa hilo kwa takribani miaka 30.

Wakazi wa mitaa mbalimbali ya mji mkuu wa Chad, – N’Djamena wameanza kusherehekea ushindi huo wa Rais Deby.