Ajali ya treni yaua 11 Misri

0
126

Watu 11 wamefariki dunia na wengine 98 wamejeruhiwa katika ajali ya treni iliyotokea karibu na mji mkuu wa Misri, -Cairo.

Mamlaka ya Reli nchini Misri imesema kuwa, treni hiyo iliyokuwa na mabehewa manne ilikuwa ikisafiri kutoka Cairo kuelekea jimbo la Mansoura na ndipo ilipoacha njia na kuanguka.

Kufuatia ajali hiyo, dereva wa treni hiyo pamoja na wasaidizi wake nane wamekamatwa na uchunguzi zaidi kubaini chanzo cha ajali hiyo unaendelea.

Habari zaidi kutoka nchini Misri zinaeleza kuwa, nchi hiyo imekuwa ikishuhudia ajali za mara kwa mara za treni.

Wiki iliyopita watu 15 walijeruhiwa baada ya treni nyingine kuacha njia na kuanguka katika jimbo la Minya al-Qamh na Machi 26 mwaka huu treni mbili za abiria ziligongana kusini mwa Misri na kusababisha vifo vya watu 19.

Mwezi Februari mwaka 2019, ilitokea ajali nyingine ya treni nchini Misri na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 30.