Klabu ya Tottenham Hotspur ya nchini Uingereza imemfuta kazi kocha wake Jose Mourinho kutokana na mwenendo mbaya wa klabu hiyo.
Uamuzi huo umefanyika baada ya timu hiyo kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Everton Ijumaa iliyopita.
Kwa sasa mchezaji wa zamani wa Spurs, – Ryan Mason na kocha wa Huddersfield Chris Powell ndio wanaoiongoza Klabu hiyo.
Mourinho alitangazwa kuwa Meneja wa Spurs mwezi Novemba mwaka 2019, akichukua nafasi ya Mauricio Pochettino ambaye nae pia alifungashiwa virago.