Watendaji wa TBC watembelea hifadhi ya Mikumi

0
159

Watendaji wa kitengo cha habari za mtandaoni cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) (Tbconline), wamefanya ziara ya kutembelea Hifadhi ya Taifa Mikumi, kujionea vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika hifadhi hiyo.

Miongoni mwa vivutio ambavyo Watendaji hao wamejionea ni wanyama wa aina mbalimbali wakiwemo Twiga, Tembo, Swala, Viboko na Nyati.

Mmoja wa waongoza Watalii katika Hifadhi hiyo ya Mikumi VIctor Lemama amesema kuwa, katika siku za hivi karibuni wamekuwa wakipokea idadi kubwa ya watalii, wengi wakiwa kutoka nchini Russia.

Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ilianzishwa mwaka 1964 ikiwa na Kilomita za mrada 1, 070, na ilipofika mwaka 1975 eneo la hifadhi hiyo liliongezwa na kufikia kilomita za mraba 3,230.