Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amesema mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga utaanza rasmi mwezi huu.
Akijibu swali Bungeni jijini Dodoma Dkt Kalemani amesema kuwa, mradi huo unatarajiwa kutoa ajira zaidi ya elfu 10.
Amesema utiaji saini mkataba wa utekelezaji wa mradi huo tayari umefanyika na kuwataka Watanzania kuchangamkia fursa hizo za ajira.