ACT Wazalendo yaichambua ripoti ya CAG

0
247

Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, – Zitto Kabwe ametoa wito kwa Watendaji wa Serikali kuongeza uadilifu na uzalendo katika usimamizi na matumizi ya fedha za umma, ili fedha hizo zitumike kwa malengo ya yaliyokusudiwa.
 
Zitto ametoa wito huo mkoani Dar es salaam wakati wa mkutano wake na Waandishi wa habari.

Mkutano huo ulikuwa ni kwa ajili ya kutoa taarifa ya uchambuzi wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) uliofanywa na chama hicho cha ACT Wazalendo.

 Pia ametoa wito kwa vyama vya siasa nchini kuwa mfano katika kusimamia matumizi ya fedha, ili kuepuka kupata hati chafu ambazo huvitia doa vyama hivyo.