Rais Samia Suluhu Hassan aelekea Uganda

0
565

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameondoka nchini leo kwenda nchini Uganda, kwa ziara ya kikazi ya siku moja kwa mwaliko wa Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo.

Akiwa nchini Uganda pamoja na mambo mengine, Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mwenyeji wake Rais Museveni, watahudhuria hafla na kushuhudia utiaji saini wa mkataba kati ya Serikali ya Uganda na Kampuni ya Mafuta Ghafi ya Afrika Mashariki (EACOP) juu ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la kutoka Hoima nchini Uganda kwenda Tanga nchini Tanzania.