Akata kucha baada ya kuzifuga kwa miaka 28

0
274

Ayanna Williams mkazi wa Texas nchini Marekani ameamua kukata kucha zake zilizomfanya aingie kwenye rekodi ya dunia ya mtu mwenye kucha ndefu zaidi za mikononi.

Kucha za Ayanna zimefugwa kwa zaidi ya miaka 28, na mara ya mwisho.zilipopimwa zilikuwa na urefu wa sentimeta 733.55 sawa na futi 24.

Daktari bingwa wa huko Texas, – Allison Readinger ndiye aliyekata kucha hizo za Ayanna kwa kutumia kifaa maalum.

Ayanna amesema ameamua kukata kucha hizo kwa kuwa amezichoka na anataka kuwa na maisha mapya, na kwamba sasa ndio muda muafaka wa kukata kucha hizo japo anajua kuwa atazikumbuka.

Kwa mujibu wa rekodi ya dunia ya Guinness, Ayanna Willims alivunja rekodi ya kuwa binadamu mwenye kucha ndefu zaidi duniani mwaka 2017, ambapo kucha hizo zilikuwa na urefu wa futi 19, hali iliyosababisha awe anatumia saa 20 kuzisafisha.