Mume wa Malkia Elizabeth II afariki Dunia

0
181

Prince Philip, mume wa Malikia Elizabeth amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 99 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali moja nchini humo.

Taarifa kutoka katika jumba la kifalme la Buckingham imesema, “Kwa masikitiko makubwa Malikia anatangaza kifo cha mume wake mpendwa Prince Philip, Duke wa Edinburgh.”

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Prince Philip amefariki dunia asubuhi ya leo katika nyumba ya kifalme ya Windsor Castle.

Hata hivyo taarifa zaidi zitaendelea kutolewa na familia ya kifalme ambapo wanafamilia na wananchi wa Uingereza wanaungana na waombolezaji wengine kumkumbuka Prince Philip.

Kufuatia tangazo hilo la kifo, bendera zote za mataifa yaliyo chini ya himaya ya kifalme zitapepea nusu mlingoti katika kipindi chote cha maombolezo ya kifo cha Prince Philip.

Katika siku za hivi karibuni afya ya Mfalme huyo wa Uingereza haikuwa ya kuridhisha ambapo alitangaza kujiondoa kushiriki hafla zote za kifalme.