Simba kusaka heshima mbele ya Ahly kesho

0
297

Kikosi cha Simba kipo chini Misri tayari kwa mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly utakaopigwa siku ya kesho Ijumaa.

Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema mchezo wao dhidi ya Al Ahly utakuwa wa kulinda heshima kwani tayari wametinga robo fainali ya michuano hiyo.

“Licha ya kufuzu nataka kuweka heshima ya kutokufungwa katika hatua ya makundi ndio maana nimeondoka na nyota wote,” amesema Gomes.

Simba inaongoza Kundi A ikiwa na alama 13 ikifuatiwa na Al Ahly yenye alama 8, AS Vita ina alama 4 nafasi ya tatu na Al Merrikh ina alama 2 ikiburuza mkia.

Simba na Al Ahly tayari zimefuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.