Serikali kutobadili adhabu wanaokiuka sheria za barabarani

0
186

Serikali imesema haiwezi kubadili adhabu kwa wanaokiuka sheria za usalama barabarani kwa kigezo cha kuangalia idadi ya abiria.

Akijibu swali la Mbunge wa Musoma Mjini Vedasto Mathayo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Khamis Hamza Chilo amesema kwa sasa Serikali haina mpango wa kubadili sheria hiyo kwani pamoja na kuwepo kwa faini ya shilingi elfu 30 kwa kila chombo cha usafiri kinachofanya makosa, bado matukio ya ukiukwaji wa sheria yanaendelea kutokea.

“Serikali katika hili bado haijaona haja ya kubadili sheria, hizi 30,000 zilizowekwa bado matukio yanatokea, na sisi lengo letu sio kumkomoa mwananchi,” amesema Naibu Waziri Chilo.

Amesema ni wajibu wa kila mtumiaji wa chombo cha usafiri kufuata sheria, ili kupunguza ajali za barabarani.