Televisheni za mtandaoni tu ndizo zitakazofunguliwa

0
151

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, amefafanua taarifa ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoitoa hivi karibuni kuhusu kufunguliwa kwa vyombo vya habari vilivyofungiwa.

Msigwa amesema Rais Samia Suluhu Hassan, ameelekeza Televisheni za Mtandaoni (Online Tv) tu ndio zifunguliwe na sio vyombo vya habari vingine yakiwemo Magazeti yaliyofungwa kwa mujibu wa Sheria.