Waziri Mkuu atoa maagizo kwa walioapishwa

0
291

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu wa wizara na wakuu wa taasisi walioapishwa leo kuelewa majukumu yao na kujipanga kuwatumikia Watanzania.

Akizungumza mara baada ya viongozi hao kuapa mbele ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam, amesema ni lazima wasimame kwenye nafasi zao kuhakikisha uchumi unakua.

Amesema tayari nchi imefanikiwa kuingia katika kundi la nchi zenye uchumi kati, hivyo hatua iliyobaki ni kufikisha maendeleo kwa mwananchi mmoja mmoja.

Ametumia jukwaa hilo kuwapongeza wote walioteuliwa na kuapishwa, na amewatakia utendaji kazi bora wenye tija na maslahi kwa wananchi.