Watanzania watakiwa kumuezi JPM kwa kufanya kazi

0
186

Wakristo wametakiwa kumuombea Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine ili kumuenzi aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli

Hayo yamesemwa na Mchungaji wa KKKT-Usharika wa Kimara, Willbroad Mastai wakati wa maadhimisho ya Sikukuu ya Pasaka ikiwa ni kukumbuka kufufuka kwa Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita.

Mchungaji Mastai amesema watanzania na dunia ilishuhudia kuguswa na msiba wa Hayati Dkt Magufuli na kusisitiza njia pekee ya kumuenzi ni kuendeleza yale yote mazuri aliyokuwa ameanzisha.

Aidha, ameongeza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameanza vyema katika uongozi wake na kwamba amejenga matumaini makubwa kwa watanzania katika uongozi wake

“Naamini Rais Samia Suluhu Hassan ameona mengi wakati wa msiba kwa namna Watanzania walivyomlilia aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa yale aliyoona naamini ana mengi ya kumfanya ajue Watanzania wanataka nini,” ameongeza Mchungaji Mastai

Mastai amesema kupitia salamu za Sikukuu ya Pasaka kupitia mtandao wa twitter alizotoa Rais Samia Suluhu Hassan ni ishara kubwa ya kuwaweka Watanzania Pamoja na kushirikiana katika ustawi wa Taifa la Tanzania