Dkt. Mpango athibitishwa kuwa Makamu wa Rais

0
175

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitisha aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais mteule.

Dkt. Mpango amethibitishwa na Bunge kwa asilimia 100 baada ya wabunge wote waliokuwepo Bungeni 363 kumpigia kura za ndio na hivyo kumthibitisha kuwa makamu wa Rais Mteule.

Awali Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kupitia kwa mpambe wake Kanali Nyamburi Mashauri amewasilisha jina la Dkt. Mpango bungeni ili aweze kupigiwa kura na kuthibitishwa kuwa Makamu wa Rais.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 Ibara ya 71 uthibitishisho huo wa Dkt. Mpango anavua nyadhifa zote ikiwemo ya Ubunge.