Tahasusi ‘combinations’ mpya za kidato cha 5

0
179

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetangaza tahasusi (combinations) mpya tano ambazo zitaanza kutolewa kwa wanafunzi wa kidato cha tano katika baadhi ya shule kuanzia mwaka huu.

Taarifa ya TAMISEMI imezitaja tahasusi hizo kuwa ni Physics, Mathematics Computer Studies ambayo itatolewa Shule ya Sekondari ya Wasichana Dodoma na Iyunga TEC (wavulana).

Nyingine ni Kiswahili, French, Chinese na Kiswahili, English, Chinese ambazo zitatolewa Shule ya Sekondari Morogoro (wasichana) na Shule ya Sekondari Usagara (wavulana).

Physical Education, Biology, Fine Arts na Physical Education Geography, Economics ni tahasusi nyingine ambazo zitatolewa Shule ya Sekondari Makambako (wasichana), Shule ya Sekondari Kibiti (wavulana) na Shule ya Sekondari Mpwapwa yenye mchanganyiko wa wavulana na wasichana.

Mabadiliko hayo yanalenga kuendana na mabadiliko ya dunia ili kupanua wigo wa wahitimu katika soko la ajira na kujiajiri.