Wahitimu kidato cha IV warahisishiwa kubadili tahasusi

0
168

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo, ametangaza utaratibu wa wahitimu wa kidato cha nne, 2020 kubadilisha tahasusi (combination) za kidato cha tano na kozi za vyuo vya elimu ya ufundi kwa njia ya mtandao kwenye mfumo wa kielektroniki wa uchaguzi wa kidato cha tano na vyuo mwaka 2021.

Wanafunzi wanaotaka kufanya mabadiliko wanatakiwa kuingia kwenye mfumo wa uchaguzi wa wanafunzi unaopatikana katika anuani ya selform.tamisemi.go.tz na kufuata maelekezo katika tovuti hiyo. Zoezi hili limeanza leo Machi 29 hadi Aprili 11 saa sita usiku.