Mkurugenzi Mkuu wa TPA asimamishwa kazi

0
223

Rais Samia Suluhu Hassan amemsimisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania ( TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko.

Rais Samia amechukua hatua hiyo muda mfupi baada ya kupokea taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020 Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Miongoni mwa mambo yaliyobainishwa ndani ya taarifa hiyo ni ubadhirifu mkubwa wa fedha ndani ya Mamlaka hiyo.

Rais Samia ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kufanya uchunguzi zaidi TPA ili wale wote waliohusika na ubadhirifu huo wachukuliwe hatua.