Jenerali Mabeyo : Dkt Magufuli aliamini vita ya kiuchumi ni ngumu

0
240

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo amesema mchango mkubwa uliotolewa na aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama utaendelea kuwa alama isiyofutika.

Amesema katika uhai wake Dkt Magufuli alivipenda vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama na aliviwezesha ili viweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Akitoa salamu za vyombo vya Ulinzi na Usalama katika uwanja wa Magufuli wilayani Chato mkoani Geita inapofanyika Misa Takatifu ya Mazishi ya Dkt Magufuli, Jenerali Mabeyo amesema  Dkt Magufuli alivishirikisha vyombo hivyo katika miradi mikubwa ya kiuchumi akimini kuwa vita ya kiuchumi ni ngumu tofauti na  vita nyingine yoyote.

Amemuhakikishia Rais Samia Suluhu Hassan kuwa, vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama nchini vitaendelea na jukumu la kuwalinda Watanzania na mali zao pamoja na Rasilimali zote za Taifa.

Pia amewahakikishia Watanzania  kuwa nchi na mipaka yake iko salama, na itaendelea kuwa salama.