XI JINPING AMLILIA JPM

0
309

Rais wa Jamhuri ya watu wa china XI Jinping ametuma salamu zake za pole kwa Rais Samia Suluhu Hassan kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kilichotokea Machi 17 2021.
Katika barua yake ya kiserikali Rais XI Jinping amesema amepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Hayati Dkt John Pombe Magufuli na kwa niaba ya serikali , watu wa china na yeye binafsi anatoa salamu za rambirambi kwa familia serikali na watanzania kwa ujumla kufuatia msiba huo
Amemuelezea Rais Magufuli kama kiongozi maarufu kwa Tanzania na Afrika ambaye aliwaongoza watu wa Tanzania kulinda hadhi ya nchi yao dhid ya kuingiliwa na mataifa ya kigeni na kuipatia maendeleo yanayoendana na hali halisi ya Tanzania
Aidha Rais XI Jinping amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku akiongeza kuwa China inajivunia urafiki wa muda mrefu na Tanzania na itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukuza urafiki huo katika kiwango cha juu kwa maslahi mapana ya pande zote mbili