Dkt Magufuli aliiunganisha Tanzania na Comoro

0
200

Rais Azali Assoumani wa Comoro amesema kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli ni pigo kubwa kwa nchi yake, kwani alisaidia kuiunganisha Comoro na Tanzania katika masuala mbalimbali ya maendeleo.

Amesema mataifa ya Tanzania na Comoro yana mambo mengi yanayofanana kihistoria, hivyo Dkt. MagufuliI daima aliendelea kuimarisha mshikamano na upendo baina ya mataifa hayo.

Amesema kifo cha Dkt. Magufuli si pigo kwa Tanzania pekee, bali kwa Bara lote la Afrika na dunia nzima kwani siku zote kiongozi huyo alikuwa akipigania demokrasia na uhuru wa kila Mwafrika.